Zuchu na Diamond wameachana

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Tanzania Zuhura Othman maarufu kama Zuchu ametangaza kwamba yeye na mwanamuziki mwenza wameamua kuachana rasmi.

Aliandika hayo kwenye akaunti yake ya Instagram na yamethibitishwa na Wasafi Media inayomilikiwa na Diamond Platnumz kwa kuchapisha pia kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

“Baada ya miaka mitatu ya kuwa kwenye mahusiano mimi na Nasib (Diamond Platnumz) Tumeamua Kuachana Rasmi!” aliandika Zuchu huku akisema kwamba yeye na Diamond walikubaliana kuachana.

“Tuna kazi ya pamoja ambayo tumefanya, hivyo msije kushangaa itakapoachiwa.” aliendelea kusema nyota huyo wa Bongo Fleva isijulikane kama ni kiki ya kutangaza kazi hiyo.

Alisema pia kwamba anamtakia Diamond kila la kheri lakini “Pia nawaomba watu wangu muendelee kuniunga mkono ikiwa sasa mwelekeo wangu ni kujiponya majeraha ya mapenzi.”

Zuchu alisema pia kwamba anaangazia kuongeza utendakazi wake katka muziki.

Ujumbe huo wa Zuchu umepachikwa kwenye Insta Stories za Diamond Platnumz ila yeye mwenyewe hajatoa taarifa rasmi kuhusu utengano wao.

Share This Article