Zuchu amiminia Diamond maneno matamu kwenye siku yake ya kuzaliwa

Marion Bosire
2 Min Read

Zuhura Othman maarufu kama Zuchu mwanamuziki wa Tanzania amemimina maneno matamu kwa mume wake ambaye pia ni mwanamuziki mwenza Diamond Platnumz.

Zuchu alitumia akaunti yake ya Instagram iliyo na wafuasi wapatao milioni 7 kuwasilisha ujumbe wa heri njema kwa mume wake ambapo alichapisha picha na video kadhaa za pamoja.

Katika moja ya video hizo, Diamond ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul anaonekana akiwa ameketi kitandani akiwa na zawadi kadhaa uso wake ukiwa umejaa furaha.

“Leo Kazaliwa Kiboko yangu ,Boss wangu ,Hero wangu ,Mentor wangu ,Msimamizi wangu ,Danga Langu ,Last say wangu ,Muchuchu wangu ,boyfriend,MUMEWANGU” aliandika Zuchu.

Wawili hao walifunga ndoa mwezi Aprili mwaka huu lakini wakaamua kutangaza kwa umma mwezi Juni.

“Ninapoahidi kuendelea kuwasha moto kichwa chako na kukukera milele, nataka pia nikutakie siku njema ya kuzaliwa mpenzi wango” aliendelea kusema binti yake Khadija Kopa.

Zuchu aliendelea kumwambia Diamond kwamba penzi lao ni la humu duniani na hata baadaye akimtaka ajiandae kisaikolojia.

“Nakupenda mume wangu furahia siku yako huku ukikumbuka kua You are The Goat ..And oh i remembered pls Return My gifts you already have me so You really don’t need any ” alimalizia.

Huku haya yakijiri, Diamond yuko kazini kama kawaida ambapo anatumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Arusha.

Diamond alizaliwa Oktoba 2, 1989 na ametimiza umri wa miaka 36. Mwanawe wa kiume aliyejaliwa na mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna naye alizaliwa Oktoba 2, 2019 na ametimiza umri wa miaka 6.

Mamake alimwandalia sherehe shuleni leo ambapo alisherehekea pamoja na wenzake akisema kwamba keki iliyokatwa ni ya kwanza kati ya nne ambazo amempangia.

Kulingana na machapisho kwenye akaunti ya Instagram ya Naseeb Junior, keki ya pili itakatiwa nyumbani labda baada yake kutoka shuleni.

Share This Article