Zoezi la Utoaji chanjo kudhibiti magonjwa ya Mifugo, asema Rais

Francis Ngala
1 Min Read

Rais William Ruto amesema zoezi la utoaji chanjo ya mifugo linanuia kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini,na kuhakikisha afya ya mnyama inabaki salama.

Katika taarifa kupitia mtandao wa X, zamani ukiitwa Twitter, Rais William Ruto amebainisha kuwa zoezi hilo litaendeshwa kwa utaratibu sahihi ili kufikia maeneo yote ya nchi.

“Mpango wa chanjo ya mifugo tutakaouanzisha Januari 2025 unakusudiwa kudhibiti ipasavyo magonjwa ya mifugo na kuhakikisha mifugo yenye afya salama, Rais Ruto aliandika kwenye mtandao wake wa X huku akitaja changamoto ambazo awali zimechangia zoezi hili kukosa ufanisi.

“Awali, zoezi hili halikuwa na ufanisi kwa sababu lilifanyika tu katika baadhi ya sehemu”, akaeleza.

Kwenye Mpango huu mpya wa utoaji chanjo ya mifugo, Ng’ombe Milioni 22 zitapokea chanjo hiyo ambayo itaanza kutolewa mapema mwakani.

“Chini ya mpango huu mpya (wa utoaji Chanjo ya Mifugo), ng’ombe milioni 22, kondoo na mbuzi milioni 50 katika maeneo yote ya nchi yetu watafikiwa na chanjo hiyo” Rais William Ruto.

Aidha Rais William Ruto amesema mpango huu utakuwa na tija kwa taifa na wafugaji kwa ujumla. “Utakuwa mwanzo wa uwekezaji zaidi wa serikali katika sekta ya mifugo ili kuifanya kufikia uwezo wake mkubwa na kutoa mchango wake kamili katika uchumi”

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.