Zaidi ya wanariadha 400 wajiandikisha kwa mbio za nyika za Roysambu United

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya wanariadha 400 wamejisajili kwa makala ya kwanza ya mbio za kuhifadhi mazingira za Roysambu United, zitakazoandaliwa Ijumaa hii uwanjani Kasarani.

Mbio hizo zitakuwa za vityengo vya kilomita 10 kwa wanaume na wanawake, kilomita 8 na 6 kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, na mbio za watoto na wakongwe huku usajili ukitarajiwa kufungwa rasmi Alhamisi hii.

Mwandalizi wa mbio Dkt Faith Mwaura amesema lengo ni kuhamasisha umuhimu wa utunzaji mazingira na pia kuchangisha hela za kuwalipia karo watoto kutoka kwa jamii zisizojimudu katika jamii.

Washindi wa kilomita 10 watatuzwa shilingi 40,000, nafasi za pili 25,000, huku watakaomaliza katika nafasi za tatu wakitia kibindoni shilingi 15,000.

Washindi wa kilomita 8, wavulana na wasichana, watapokea shilingi 10,000 huku washindi wa kilomita 12, wanawake na wanaume, wakipokea shilingi 12,000 kila mmoja.

Aidha, chama cha Riadha Kenya tawi la Nairobi litatumia mashindano hayo kuchagua kikosi kitakachoakilisha eneo hilo kwenye mbio za kitaifa za nyika tarehe 25 mwezi huu jijini Eldoret.

Share This Article