Wanabodaboda zaidi ya 200 wapokea pikipiki za umeme eneo bunge la Mwala

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanabodaboda zaidi ya 200 katika eneo bunge la Mwala, kaunti ya Machakos, walipokea walipigwa jeki kwa kupokea pikipiki mpya za umeme katika mradi wa kuwainua kiuchumi wakazi wa eneo hilo na kubadilisha sekta hiyo ya uchukuzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mapema wiki hii katika uwanja wa Masii mbunge wa eneo hilo Vincent Kawaya,alisema wakazi watahitajika kulipa ada ya shilingi 180 kwa siku kwa mwaka mmoja unusu ili kumiliki pikipiki hizo.

Kawaya aliwashutumu baadhi ya wafanya biashara wanaowapunja wananchi kwa kuwauzia pikipiki kwa bei ghali hali inayolemaza kichumi.

Mbunge pia alitangaza mipango ya kujenga vidanda kwa waendeshaji pikipiki katika eneobunge la mwala huku 1500, wakipokea mafunzo ya kitaalam ya kuendesha pikipiki na kupewa leseni za kidijitali za uendeshaji.

Share This Article