Klabu ya Young Africans almaarufu Yanga, imekataa kata kata kurudia kucheza derby ya Kariakoo, dhidi ya watani wa jadi klabu ya Simba.
Uongozi wa Yanga umeeleza kuwa hauna imani kabisa na mamlaka za soka nchini Tanzania kutokana na kile walichokiita uonevu, uvunjaji wa kanuni na upendeleo wa wazi unaoendelea kufanywa dhidi ya baadhi ya timu ligini humo.
Yanga imesema haiku tayari kwa marejeleo ya mechi hiyo nambari 184 amabyo haikuchezwa, na imetoa wito kwa wanachama na mashabiki wake kuwa tayari kupigania haki yao ili kukomesha .
Simba walikataa kucheza derby hiyo iliyoratibiwa tarehe 8 mwezi Machi mwaka huu, kwa kuteta kuwa wenyeji wao Yanga wakikataa kuwaruhusu kuingia uwanjani Benjamin Mkappa, ili kufanya mazoezi ya mwisho ilivyo desturi.
Yanga walikaidi kuwasilisha kesi na tetesi zao kwa usimamizi wa Ligi Kuu ya Tanzania; badala yake, wakapeleka kesi katika mahakama ya kimataifa ya kutatua migogoro michezoni (CAS).
Hata hivyo, CAS ilikataa kuskiza kesi hiyo na kuirejesha kwa wasimamizi wa Ligi.