Yanga waikwatua Simba na kutwaa Ligu Kuu Tanzania bara

Yanga walifunga msimu kwa alama 82,wakifuatwa kwa umbali na Simba kwa pointi 78, baada ya mechi 30 za msimu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Young Africans maarufu kama Yanga, ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2024/2025.

Hii ni baada ya kuwazaba watani wa jadi Simba mabao 2-0, katika mechi ya kufunga msimu iliyosakatwa katika uwanja wa taifa wa Mkappa jijini Dares Salaam,Tanzania Jumatano jioni.

Kiungo wa Ivory coast Pacome Zouzoua, alipachika goli la ufunguzi kwa Yanga, kunako dakika ya 66, baada ya kipindi cha kwanza kuishia sare tasa.

Chipukizi Clement Mzize alipachika la pili katika dakika ya 88 na kuwapa Yanga ubingwa wa nne kwa mpigo wa ligi hiyo.

Yanga walifunga msimu kwa alama 82,wakifuatwa kwa umbali na Simba kwa pointi 78, baada ya mechi 30 za msimu.

Yanga ukipenda Jangwani Boys wameshinda jumla ya mataji 26 ya Ligi Kuu Tanzania bara, huku wakiwahi tiketi ya kushiriki kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao wakiandamana na Simba wakati Azam waliomaliza wa tatu wakishiriki kombe la shirikisho.

Simba wameshinda ubingwa wa ligi hiyo mara 21, ya mwisho ikiwa msimu wa mwaka 2020/2021.

Share This Article