Wizara ya Michezo na Utamaduni inadaiwa shilingi milioni 63 na Maktaba ya Kitaifa (KNLS).
Afisa Mkuu Mtendaji wa KNLS, Dkt. Charles Nzivo, ameiambia kamati ya bunge ya michezo na utamaduni kuwa wizara ya Michezo iliyokuwa ikitumia afisi zake ilihama bila kulipa deni hilo.
Nzivo ameongeza kuwa juhudi zao za kuitaka wizara ya michezo ilipe deni hilo zimegonga mwamba.
Kamati hiyo ya bunge inayoongozwa na mbunge wa Webuye West Dan Wanyama imeambiwa kuwa KNLS kwa jumla hukusanya shilingi milioni 75 kutoka kwa kodi na nyingine milioni 20 kwa kutoa huduma kwa wateja.