Wizara ya Afya yazindua mpango wa Epuka Uchafu Afya Nyumbani, Migori

Muthoni aliwataka viongozi wa mashinani kushirikiana katika kufanikisha kuwepo kwa mazingira safi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni jana Alhamisi alizindua mpango wa kuhamasisha usafi unaojulikana kama Epuka Uchafu Afya Nyumbani, katika eneo la Apida, kaunti ya Migori.

Kampeni hiyo inahamisha jamii kudumisha usafi wa mazingira kupitia utupaji taka vizuri na usafi kwa jumla.

Muthoni, aliwataka viongozi wa mashinani kushirikiana katika kufanikisha kuwepo kwa mazingira safi.

“Tulisisitiza kuwa usafi wa mazingira unapaswa kuwa kitu cha kawaida, wala siyo shughuli ya kufanywa wakati mmoja. Mazingira safi yanasalia njia bora zaidi ya kuzuia magonjwa na kuhamasisha afya ya jamii,” alisema Katibu huyo aliyeandamana na kamisha wa kaunti ya Migori Kisilu Mutua.

Wengine waliokuwepo ni Waziri wa Afya wa kaunti hiyo Julias Nyerere na maafisa wengine waandamizi wa serikali ya Migori.

Share This Article