Wizara ya afya imezindua mitambo ya kidijitali 1,140 itakayotumiwa na wastawishaji wa afya ya jamii.
Akizindua matumizi ya mitambo hiyo leo katika kaunti ya Nakuru, Waziri wa Afya Aden Duale, amesema mashine hizo zitawasaidia wananchi kufuatilia hali zao za kiafya.
Tayari wastawishaji wa afya jamii 3,306 wamepokea mafunzo ya kutoa huduma za kiafya chini ya mpango wa Taifa Care.
Duale amesisitiza kuwa serikali itahakikisha huduma bora za kiafya.
Duale ameongeza kuwa kaunti ya Nakuru imewasajili takriban watu 840,000, kwa mpango wa SHA.