Wizara ya afya yawatimua wauguzi wanagenzi 42

Wizara ya afya imefutilia mbali barua za kazi walizopewa wanafunzi hao na kumsimamisha kazi Afisa Mkuu mtendaji wa NCK Dkt. Lister Onsongo kusubiri kufanywa kwa ukaguzi kuhusu kundi la wanagenzi.

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Mazingira Aden Duale.

Wizara ya Afya imewatimua wauguzi wanagenzi 42 kwa kukiuka sheria za taaluma hiyo kwa ushirikiano na baraza la kitaifa la  uuguzi nchini NCK.

Kulingana na taarifa iliyotiwa saini na Waziri wa Afya Aden Duale, wanagenzi hao 42, wanaosomea uuguzi katika vyuo vikuu walishirikiana na vikuu 10 vya umma na NCK na kuanza kuwaajiri wanagenzi kabla ya kukamilisha kipindi cha masomo kinachohitajika.

Wizara ya afya imefutilia mbali barua za kazi walizopewa wanafunzi hao na kumsimamisha kazi Afisa Mkuu mtendaji wa NCK Dkt. Lister Onsongo, kusubiri kufanywa kwa ukaguzi kuhusu kundi la wanagenzi ambao wameajiriwa.

Wakati uo huo Duale amemteua Bi Ann Mukuna, Mkurugenzi wa ubora wa viwango, kusimamia baraza hilo hadi uchunguzi utakapokamilika.

 

Share This Article