Willy Paul amjibu Patelo

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki Willy Paul amemjibu VJ Patelo kwa njia ambayo wengi hawangetarajia baada ya Patelo kumzomea kwenye video aliyochapisha katika akaunti yake ya Tiktok.

Katika video hiyo, Patelo anamtupia Willy Paul maneno makali kwa kukosa kuwajibija jinsi alikuwa ameahidi kabla yake na mke wake Diana au ukipenda Dee kukubali kuonekana kwenye video yake.

“Usiwahi nipigia simu kama huwezi fika bei, msanii kama Willy Paul. Wewe ni msanii mgani sasa? Unaniita nitokee kwa shughuli yako ukiniambia vile unaweza weka ngata ushughulike …” alilalamika Patelo.

Aliendelea kulalamika kwamba Willy Paul hakumlipa walivyokubaliana akisema heri angemwambia ukweli kwamba hawezi kumlipa atokee tu kama rafiki.

Willy Paul alichapisha kipande cha video ya wimbo wake ambapo Patelo na Dee wanaonekana akiwataja kuwa watu wake wa maana sana.

“Patelo na Diana Dee ndio watu ninawapenda sana kwa wakati huu. Ni visanga tu za waliozidi umri wa miaka 18 sio walio chini ya umri wa miaka 18. Waangalie manze” aliandika Willy Paul.

Hata hivyo hakusema lolote kuhusu lalama za Patelo na hivyo haijulikani iwapo aliwalipa au hakuwalipa kwa kuonekana kwenye video yake.

Share This Article