Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), limetangaza kuwatimua nusu ya wafanyakazi wake kutokana na hatua ya Marekani kuondoa ufadhili wake .
Aidha, WHO, litalazimika kupunguza kabisa shughuli zake kote duniani kutokana na uchechefu wa pesa huku pia likitangaza kufunga baadhi ya afisi zake katika nchi zenye kipato cha juu.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Gebrejesus, alisema juzi kuwa wamepunguza bajeti yao kwa asilimia 21 kutokana na hatua hiyo ya Rais Donald Trump, ya Januari 20, mwaka huu.
Timu ya uongozi ya WHO, ambayo kwa kawaida imekuwa na maafisa 14, akiwemo Gebrejesus, imepunguzwa hadi saba,
WHO, imedokeza kuwa itarejelea hali yake ya kawaida endapo mataifa wanachama yatakubali kuongeza kiwango cha pesa wanazolipa kwa sasa.