Wendy Williams aonekana mwenye furaha

Alikuwa amewasili Miami, Florida kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya babake.

Marion Bosire
2 Min Read

Mtangazaji wa Marekani Wendy Williams alionekana mwenye furaha katika uwanja wa ndege huko Miami, ikiaminika kwamba ni kutokana na hatua ya kubadilisha mazingira.

Williams anaishi katika makazi yenye masharti mengi huko New York alikopelekwa na usimamizi wake wa kisheria na huwa haruhusiwi kuonana na watu wa familia yake.

Jaji alimruhusu ahudhurie sherehe ya siku maadhimisho ya kuzaliwa kwa babake mzazi ndiposa huko Florida na alinaswa kwenye video muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Miami.

Wendy alikuwa anatumia skuta yake na kwenye video anasikika akiangua kicheko ila hakusema na wanahabari waliokuwepo.

Alikuwa akinong’onezana na wasaidizi wake pamoja na mlinzi ambapo aliwaambia alikuwa anahisi njaa na angependa kupata kitu cha kula. Alichukua pia simu na kuzungmza na mtu asiyefahamika kabla ya kuabiri gari lililokuwa likimsubiri.

Wendy anatarajiwa kukutana na watu wa familia yake kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa, katika sherehe hiyo babake anapotimiza umri wa miaka 94.

Katika mahojiano na Harvey na wakili Mark Geragos katika kipindi cha mitandaoni, Wendy alisema anatumai kuonana na mwanawe wa kiume ambaye anamlaumu kwa kutumia vibaya pesa zake.

Kwa sasa Wendy anapambana mahakamani kutafuta kukomesha usimamizi huo wa kisheria ambao aliwekewa baada ya madai kwamba alikuwa akiugua ugonjwa wa akili.

Katika mahojiano hayo Wendy alisikika na kuonekana timamu huku wadadisi wakihisi kwamba alilazimika kujisingizia ugonjwa huo awali ili kukwepa watu ambao wangetaka kumdhuru.

Katika kipindi alichokuwa akiongoza cha runinga, Wendy alikuwa akifichua mambo kadhaa yanayoweza kuchukuliwa kuwa siri za watu maarufu na wenye ushawishi mkubwa.

Mmoja wa watu hao anadaiwa kuwa P. Diddy ambaye yuko kizuizini na inaripotiwa kwamba ndiyo sababu sasa Wendy anataka uhuru wake.

Share This Article