Waziri Ogamba akanusha madai ya kuongeza alama za kujiunga na vyuo vikuu

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa elimu Julius Ogamba.

Waziri wa Elimu Julius Ogamba amekanusha madai kwamba wanafunzi waliopata alama ya C+ mwaka uliopita hawatajiunga na vyuo vikuu.

Ogamba amesisitiza kuwa alama za chini za kujiunga na vyuo vikuu bado ni C+ ilivyotangazwa awali.

Ameongeza kuwa wanafunzi wote 246,391, waliopata alama ya C+ na zaidi katika mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka jana, watajiung na vyuo vikuu.

Waziri amefichua kuwa mtandao wa wanafunzi kuchagua kozi, KUCCPS utafunguliwa mwezi ujao.

Share This Article