Waziri Mvurya akabidhi uwanja wa Kasarani kwa kamati ya CHAN

Uga huo utaandaa mechi zote za Harambee Stars za kundi A pamoja na fainali ya kipute cha CHAN Agosti 30.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Michezo Salim Mvurya, siku ya Jumatatu amekabidhi rasmi uwanja wa Kasarani kwa kamati andalizi ya fainali za nane za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanandinga wa ligi za nyumbani (CHAN).

Hii ni baada ya kukamilika kwa ukarabati ambao umekuwa ukifanyiwa uwanja huo kwa muda mrefu.

Uga huo utaandaa mechi zote za Harambee Stars za kundi A pamoja na fainali ya kipute cha CHAN Agosti 30.

Wenyeji wa Tanzania watafungua kipute hicho kundini B katika uchanjaa wa Benjamin Mkapa tarehe 3 Agosti dhidi ya Burkina Faso.

Mechi nyingine za kundi A zitachezewa katika uga wa kitaifa wa Nyayo.

Mataifa 19 yaliyogawanywa kwa makundi manne yatashiriki fainali hizo.

Share This Article