Waziri Mkuu wa Lithuania ajiuzulu

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Lithuania Gintautas Paluckas ambaye amejiuzulu

Waziri Mkuu wa Lithuania Gintautas Paluckas alijiuzulu leo Alhamisi huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na uwezekano wa kutekelezwa kwa uhalifi wa kifedha uliofanywa na kampuni zinazohusishwa naye.

“Nilimtaarifu Rais karibu saa moja iliyopita kwamba nimefanya uamuzi wa kujiuzulu kama Waziri Mkuu,” Paluckas alisema kwenye taarifa.

Pia alisema anajiuzulu wadhifa wake kama mkuu wa chama cha Social Democratic.

“Licha ya uamuzi wangu wa kuacha majukumu yangu ya sasa, nitaendelea kulinda heshima na hadhi yangu na ninasubiri kumalizika kwa uchunguzi, ambao nina hakika utatenganisha ukweli na madai,” aliongeza Paluckas.

Share This Article