Waziri wa Kilimo amenza ziara ya wiki moja nchini Marekani kwa lengo la kupata soko la moja kwa moja kwa bidhaa za kilimo za Kenya nchini humo.
Siku ya kwanza ya ziara yake, Kagwe na ujumbe wake ulikutana na uongozi wa duka kubwa la rejareja la Walmart, linaloendesha zaidi ya maduka 40,000 kote nchini Marekani ili kufungua milango ya kuuzwa kwa chai ya Kenya, makadamia na bidhaa zingine nchini humo.

Wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa MACNUT Jane Maigua alinadi makadamia ya Kenya kama bidhaa bora inayokuzwa kwa njia asilia bila matumizi ya kemikali.
Ziara hiyo itajumuisha mazungumzo na Wizara ya Biashara na ile ya Kilimo ya Marekani na sekta binafsi miongoni mwa wadau wengine.
Akiwa katika jimbo la South Carolina, Waziri Kagwe alifanya mazungumzo na kampuni ya chai ya Milo ambayo ni mzalishaji kinara wa chai ya barafu nchini Marekani’.
Ziara hiyo inaashiria juhudi za nchi hii za kushinikiza uuzaji wa bidhaa za Kenya moja kwa moja nchini Marekani.