Waziri wa kilimo na ustawishaji wa mifugo Mutahi Kagwe, amekariri kujiotolea kwa serikali kuimarisha ushirikiano na Uholanzi, ili kuongeza tija katika kilimo cha humu nchini.
Waziri Kagwe alisema haya jana wakati wa sherehe ya mapokezi ya kibalozi iliyoandaliwa na balozi wa Uholanzi nchini Kenya, Henk Jan Bakker, kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mfalme Willem-Alexander .
Sherehe hiyo iliyoandaliwa kwenye makazi ya Balozi wa Uhonzi nchini Kenya, ilidhihirisha ushirikiano wa zaidi ya miongo sita kati ya Kenya na Uholanzi, hususan katika sekta ya kilimo.