Wawili wahofiwa kufariki baada ya ndege ya jeshi kuanguka Kwale

Dismas Otuke
1 Min Read

Marubani wawili wanahofiwa kufariki kufuatia kuanguka kwa ndege ya jeshi aina ya Kenya Airforce Grob 120A,  katika shule ya msingi ya Mwakijembe, Ndavaya,kaunti ya  Kwale.

Kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya jeshi nchini ndege hiyo ya mafunzo, ilianguka mapema leo baada ya kukumbwa na dharura.

Waliofariki ni pamoja na rubani na mwanafunzi aliyekuwa akipewa mafunzo.

Ndege iliondoka Mombasa saa tano na dakika 39 asubuhi, na kuonekana kwa mara ya mwisho karibu na Diani kabla ya kutoweka katika mtambo wa Radar na iliripotiwa kuanguka dakika 27 baadaye

 

TAGGED:
Share This Article