Wawili wafariki, kadhaa wajeruhiwa ajali ya Mai Mahiu

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu wawili wameripotiwa kufariki Jumamosi usiku kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Mai Mahiu kwenye barabara ya kuelekea Narok.

Ajali hiyo ilihusisha basi la Ena Coach lililogongwa na trela ambalo dereva wake alipoteza mwelekeo.

Yamkini watu kadhaa wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha baada ya kujeruhiwa.

Basi la kampuni ya Ena Coach, lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea Kehancha, lilipinduka baada ya kugongwa kutoka nyuma na trela.

 

TAGGED:
Share This Article