Watu wanne wamefariki kwenye ajali ya barabarani iliyotokea Jumamosi asubuhi katika kaunti ya Kiambu.
Kulingana na polisi, ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Northern Bypass karibu na daraja la Membley saa kumi alfajiri.
Akithibitisha ajali hiyo, kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Ruiru Charles Kibathi, alisema ajali hiyo ilihusisha magari mawili, gari ndogo aina ya Suzuki na trela, zote zikielekea upande mmoja.
Kulingana na Kibathi, gari hilo aina ya Suzuki lilipoteza mwelekeo na kuligonga trela upande wa nyuma kwa kishindo na kusababisha vifo vya watu wanne wote waliokuwa kwa gari hilo ndogo.
” Watu wote wanne waliokuwa ndani ya Suzuki, wanawake watatu na mwananume mmoja waliangamia papo hapo,” alithibitisha Kibathi.
Afisa huyo wa polisi alisema ajali hiyo ilisababishwa na uendeshaji gari kwa kasi kupita kiasi, huku miili ya walioangamia ikipelekwa katika makafani ya hospitali ya rufaa na matibabu ya Kenyatta