Angaa watu kumi waliripotiwa kuaga dunia baada ya kuporomokewa na mgodi wa dhahabu walimokuwa eneo la South Kivu nchini DRC.
Msemaji wa kundi la waasi wa M23, linalotawala eneo hilo Douglas Dunia Masumbuko, alisema idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi huku utafutaji wa mili ukiendelea.
Aliongeza kuwa pia idadi ya amjeruhi ilikuwa nyingi kuongeza uwezekano wa vifo zaidi akilaumu hali mbaya ya mgodi huo kuwa chanzo za kuporomoka.