Idadi ya waliofariki kwenye ajali Kisumu yapanda hadi 25

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya Faith Matete

Idadi ya waliofariki kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea leo Ijumaa jioni mjini Kisumu imefikia watu 25. 

Hii ni baada ya watu wanne zaidi kufariki wakati wakipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga.

Awali, watu 21 walithibitishwa kufariki, miongoni mwao wanaume 10, wanawake 10 na mtoto mmoja msichana.

Ajali hiyo ilitokea kwenye mzunguko wa Coptic katika mtaa wa Mamboleo kwenye barabara ya Kisumu kuelekea Kakamega.

Akithibitisha ajali hiyo, Mkuu wa Polisi wa Trafiki wa eneo la Nyanza Peter Maina alisema watu 5 walijeruhiwa vibaya wakati wa ajali hiyo huku wengine 15 wakipata majeraha mbalimbali.

Miili ya waliofariki imepelekwa ili kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga.

Majeruhi pia wanatibiwa katika hospitali yiyo hiyo.

Ajali hiyo ilitokea pale basi la shule, lililokuwa limebeba waombolezaji, lilipoanguka mtaroni na kupinduka juu chini.

 

TAGGED:
Share This Article