Watu 10 wafariki kwenye mlipuko wa gari nchini India

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu kumi wafariki kwenye mlipuko nchini India. Picha/Hisani.

Takriban watu kumi wamefariki Jumatatu jioni, baada ya  gari kulipuka katika mji mkuu wa India, Delhi.

Video zilizosambaa zilionyesha moshi mkubwa ukifuka, huku magari kadhaa yakiwa yameharibiwa vibaya, huku maafisa wa huduma ya kwanza wakiwasaidia wahasiriwa.

Chanzo za mlipuko huo hakikujulikana mara moja, lakini, huku Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akitaja tukio hilo kuwa la kuhuzunisha.

“Nimezungumza na asasi zote zinazochunguza kisa hicho…..wale wote waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria,’ alisema Modi.

Waziri wa ulinzi wa India Rajnath Singh   kupitia ukurasa wa X, alisema matokeo ya uchunguzi huo yatawekwa wazi na waliohusika katika mkasa huo hawatasamehewa.

“Nahakikishia taifa hili kuwa wale wote waliotekelezwa uovu huo hawatasazwa kwa vyovyote vile,” alidokeza Singh.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah na maafisa wengine wamesema “wanachunguza uwezekano wote ” juu ya kile ambacho kumesababisha mlipuko huo.

Share This Article