Zaidi ya watoto 1,200 walio chini ya umri wa miaka 14, wamenufaika kwa kupata bidhaa za usafi katika kaunti ya Machakos.
Kwenye kampeni hiyo ya wiki moja ya kupambana dhidi ya magonjwa ya ukambi na homa ya matumbo, kampuni ya Pwani Oil ilitoa mafunzo ya ki afya na pia sabuni kwa watoto hao walio chini ya umri wa miaka 14 katka kaunti ya Machakos.
Pwani Oil ilishirikiana na chama cha wauguzi nchini KPNA, wizara ya afya na serikali ya kaunti ya Machakos ilizindua mpango wa uhamasisho kuhusu wa magonjwa ya ukambi na kifua kikuu katika hospitali ya Machakos Level 5.
Kampeini hiyo ilishirikisha mpango wa usafi na kuzuia magonjwa ya kuambukizana katika maeneo ya mashinani nchini.