Washukiwa wawili wakamatwa wakisafirisha pembe sita za ndovu Turkana

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wakamatwa wakisafirisha pembe sita za ndovu Turkana.

Washukiwa wawili wamekamatwa wakisafirisha pembe sita za ndovu kwenye barabara ya Lodwar-Kalokol, kaunti ya Turkana.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Turkana ya kati Evans Ombui, alisema wawili hao walikamatwa baada polisi kupashwa habari na wananchi.

Pembe hizo zina uzani wa kilo 26.4, kulingana na Afisa Mkuu wa Huduma ya Taifa kwa Wanyamapori (KWS) kaunti ya Turkana, Elijah Chege.

‘Wananchi waliwajulisha maafisa wa KWS, ambao waliwahusisha maafisa wengine wa usalama na kuwatia nguvuni washukiwa hao katika eneo la  Monti takriban kilomita 45 kutoka mji wa Lodwar ,’ alisema Ombui.

Washukiwa hao watafikishwa mahakamani Jumatatu.

TAGGED:
Share This Article