Washukiwa wawili wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa Mombasa.

Maafisa wa usalama kaunti ya Mombasa, wamewakamata washukiwa wawili wa ulanguzi wa mihadarati, huku wakipatikana na misokoto kadhaa ya bangi.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kupitia ukurasa wa X, ilisema maafisa wa polisi walipokea habari kuhusu mzigo uliowasili katika enep la Mwembe Tayari kutoka Homa Bay, ambao ulitiliwa shaka.

Maafisa hao walichukua hatua na kufika katika kituo hicho cha magari na kusubiri atakayewasili kuupokea mzigo huo.

Pamela Akinyi Ochichi and Daniel Agolla Ogweno, waliwasili kupokea mzigo huo, na kutiwa nguvuni ambapo wanazuiliwa katika korokoro za polisi, wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Bangi hiyo itatumika kortini kama ushahidi dhidi yao.

TAGGED:
Share This Article