Washukiwa watatu wakamatwa kwa usambazaji wa pesa bandia

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa watatu wakamatwa kwa kujihusisha na usambazaji pesa bandia.

Washukiwa watatu wanaohusishwa na sakata ya kusambaza pesa bandia katika kaunti ya Mombasa na viunga vyake, wamekamatwa kufuatia operesheni iliyotekelezwa na maafisa wa polisi eneo la Diani.

Washukiwa hao Fadhili Lawrence, Atemba Lawrence, na Electrine Okwako, walikamatwa baada ya maafisa wa polisi kupokea habari zilizowalekeza kwenye maficho yao katika eneo la Diani, ambapo maafisa hao walipata shilingi milioni 1.7 pesa bandia.

Noti hizo bandia za shilingi elfu moja zilikuwa zimefichwa kwenye mfuko wa kipakatalishi kilichokuwa na utepe wenye nembo ya “CBK 1000,” maelezo ya kupotosha yaliyonuiwa kuashiria uhalali.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa washukiwa hao watatu ni wahusika wakuu kwenye mtandao mpana wa uhalifu unaominika kusambaza pesa bandia kwenye eneo la pwani. Washukiwa hao ambao wanazuiliwa watafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

Washukiwa hao wanazuiliwa wakisubriri kufikishwa mahakamani.

 

TAGGED:
Share This Article