Washukiwa wa utekaji nyara wa Koimburi, waachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki tatu

Jaji Carolyne Nyaguthii,ametangaza uamuzi huo Ijumaa baada ya kuangalia ushahidi na utetezi uliowasilishwa .

Dismas Otuke
1 Min Read

Washukiwa wanne wa utekaji nyara wa Mbunge wa Juja Goerge Koimburi, wameachiliwa huru leo kwa dhamana ya shilingi laki tatu kila mmoja na mahakama kuu ya Milimani au kwa bondi ya udhamini ya shilingi milioni moja.

Jaji Carolyne Nyaguthii,ametangaza uamuzi huo Ijumaa baada ya kuangalia ushahidi na utetezi uliowasilishwa .

Hata hivyo,wanne hao Peter Kiratu, David Macharia Gatana, Cyrus Kieru Muhia, na Grace Nduta Wairimu, wameachiliwa  huru kwa masharti makali ikiwemo kuzuiwa kuwasiliana na mashahidi wa kesi hiyo wala kuhitilafiana na uchunguzi wa polisi.

Kesi hiyo inahusiana na mbunge Koimburi aliyeripotiwa kupotea Mei 25 ,baada ya kuhudhuria ibada katika kanisa la Full Gospel Ebenezer eneo la Mugutha na baadaye ikaripotiwa kuwa alikuwa ametekwa nyara.

Koimburi baadaye alipatikana katika shamba moja la kahawa akiwa na majeraha.

Polisi wangali wanaendelea ma uchunguzi kubaini kiini na chanzo kwa utekaji nyara huo .

 

Share This Article