Washukiwa wa ulanguzi wa bidhaa za wanyamapori wakamatwa Embu

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa watatu wakamatwa wakiwa na pembe za ndovu, kaunti ya Embu

Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wale wa huduma za Wanyamapori nchini, wamewakamata washukiwa watatu waliokuwa wakisafirisha pembe sita za ndovu, katika eneo la Mbeere kusini, kaunti ya Embu.

Washukiwa hao Michael Kariuki Kithaka mwenye umri wa miaka 44, Morris Kariuki Njuki (45) na Margaret Syombua Mutua (46), walinaswa katika makutano ya barabara ya Siakago-Kiritiri, wakiwa na pembe hizo za ndovu zenye uzani wa kilo 48, hatua hiyo ikiwa ukiukaji wa sheria za ulizni wa wanyamapori.

Walifikishwa katika mahakama ya Siakago, na kushtakiwa kwa kumiliki bidhaa za wanyamapori bila idhini.

Mahakama iliagiza wapelekwe rumande hadi  Juni 11, 2025, huku uchunguzi ukiendelea.

TAGGED:
Share This Article