Washukiwa sita wa ujambazi wanaswa Meru

Dismas Otuke
1 Min Read

Washukiwa sita wa ujambazi wamekamatawa na maafisa kutoka idara ya ujasusi eneo la Mutuai wakishirikiana na wenzao wa kaunti ndogo ya Igembe Kaskazini, kaunti ya Meru.

Aidha, bastola mbili za aina ya Falcon, risasi tatu, na pikipiki mbili zisizo na nambari za usajili zilipatikana kutoka kwa washukiwa hao.

Polisi waliwakamata majangili hao kwenye maficho yao baada ya kuendesha msako wa wiki kadhaa.

Silaha zilizopatikana kutoka kwa washukiwa hao zimepelekwa kufanyiwa uchunguzi.

Majambazi waliotiwa mbaroni ni; Derrick Kithinji, Aaron Mwendia, Amon Muarangiri, Anthony Munene, Francis Mugambi na Ambrose Muriithi, na wako korokoroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Share This Article