Washukiwa watatu waliokuwa na silaha huko Daraja Mbili katika eneo la Mayatta B, kaunti ya Kisumu waliwaibia waombolezaji waliokuwa wakihudhuria mazishi ya marehemu Susan Achieng’ Otieno nyumbani kwake.
Polisi kutoka kituo cha Kasagam walifika nyumbani hapo haraka baada ya mmoja wa waombolezaji kuwapigia simu baada ya maji kuzidi unga.
Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS inasema wakisaidiwa na wakazi wa eneo hilo, washukiwa watatu walikamatwa huku mmoja wao akifanikiwa kutoroka.
Washukiwa walipatikana wakiwa na pikipiki moja, nambari ya usajili, KMFK 840L.

Polisi wanasema wanafuatilia vidokezo ili kuwakamata washukiwa wengine.