Washukiwa 26 wakamatwa kwa ulaghai wa stakabadhi za serikali

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa 26 wakamatwa kwa ulagahi wa stakabadhi za serikali.

Maafisa wa usalama wamewakamata washukiwa 26, wanaotuhumiwa kuendesha shughuli haramu ya utoaji stakabadhi za serikali.

Kwenye oparesheni ya pamoja iliyotekelezwa na asasi mbali mbali za usalama, washukiwa hao walikamatwa kwa madai ya utoaji kitambulisho cha kitaifa, pasispoti na cheti cha kuzaliwa.

Operesheni hiyo ya siku mbili iliwalenga wafanyakazi husika wa serikali wanaohudumu katika idara ya Usajili wa Watu, Idara ya Uhamiaji, Machifu, wafadhili na mabroka ambao ni wahusika kwenye shughuli hiyo haramu.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), watu hao hushirikiana kuepuka utaratibu wa kawaida katika kupata stakabadhi hizo bila kufuata taratibu za mifumo ya kiusalama na hivyo kutoa stakabadhi hizo kinyume na sheria.

Vifaa vya serikali vilipatikana nyumbani kwa baadhi ya washukiwa wakati wa oparesheni hiyo.

Miongoni mwa vifaa vilivyopatikana ni karatasi za kuchapishia vitambulisho vya kitaifa, vifaa vya kuchukua alama za vidole, vyeti vya kuzaliwa na kifo, pasipoti na mihuri rasmi ya serikali.

Waliokamatwa ni wafayakazi wa serikali kutoka maeneo ya Embakasi, Kamukunji, Eastleigh na wakuu wa ofisi za serikali. Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

TAGGED:
Share This Article