Jumla ya wapiga kura milioni 37,655,559, wamejiandikisha kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa nchini Tanzania Oktoba 29 mwaka huu.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 26.5 kutoka kwa idadi ya wapiga kura milioni 29.7 waliojiandikisha kwa uchaguzi wa mwaka 2020.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Jacob Mwambegele, alifichua hayo wakati wa kuzindua ratiba ya uchaguzi mkuu jijini Dodoma.
Uchaguzi huo utashirikisha Nyadhfa za Urais, Ubunge, na Udiwani.