Wanyonyi atamba London Diamond League

Wanyonyi alimshinda bingwa wa Dunia Marco Arop wa Canada, akiziparakasa kwa rekodi moja ya dakika ya 1 na sekunde 42.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 800, Emmanuel Wanyonyi, ameendeleza msururu wa matokeo mazuri baada ya kushinda mkondo wa London Diamond League Jumamosi.

Wanyonyi alimshinda bingwa wa Dunia Marco Arop wa Canada, akiziparakasa kwa rekodi moja ya dakika ya 1 na sekunde 42.

Arop amemaliza wa pili kwa muda wa dakika 1 sekunde 42.22,  huku Mwingereza Max Burgin, akiambulia nafasi ya tatu.

Margaret Akidor wa Kenya ambaye amefuzu kwa mashindano ya dunia katika mita 5,000 amemaliza katika nafasi ya  9 ya shindano hilo la mizunguko 12 unusu.

Share This Article