Wanariadha wa Kenya wamaliza wiki ya kwanza ya mazoezi

Kenya inajiandaa kushiriki makala ya 20 mashindano ya riadha duniani yataandaliwa baina ya Septemba 13 na 21.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha wa Kenya wamekamilisha wiki ya kwanza ya kambi ya mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya Riadha Duniani mwezi ujao mjini Tokyo, Japan.

Timu hiyo inahyowajumuisha wanariadha 58, imekita kambi katika kambi ya mazoezi ya nyanda za juu mjini Eldoret.

Wanariadha wa mbio za masafa ya kadri na marefu na marathon wako kambini Eldoret, huku wake wa mbio za masafa mafupi mafupi wakipiga kambi katika uwanja wa Kasarani, Nairobi.

Kenya inajiandaa kushiriki makala ya 20, ya mashindano ya riadha duniani yataandaliwa baina ya Septemba 13 na 21.

Kenya ilimaliza ya nne katika makala ya mwaka 2023 kwa medali 10, dhahabu 3, fedha 3 na shaba 4.

 

 

TAGGED:
Share This Article