Timu ya wanariadha chipikizi wa Kenya imekamilisha mazoezi yake leo kwa mashindano ya bara Afrika nchini Nigeria.
Wanariadha hao 47 wamekuwa katika kambi ya mazoezi katika uwanja wa Kasarani kujiandaa kwa mashindano hayo yatakayoandaliwa mjini Abeokuta, Nigeria, kati ya Julai 16 na 20.
Timu hiyo ilipewa motisha leo na bingwa wa Jumuiya ya Madola Ferdinand Omanyala.
Mkurugenzi wa riadha ya chipukizi Barnaba Korir,ana imani ya timu hiyo kufanya vyema huku akiwapa changamoto chipukizi hao kujitoa mhanga.
Kenya ilimaliza ya tatu katika makala ya mwaka 2023, mjini Ndola, Zambia; kikosi cha chipukizi chini ya umri wa miaka 20, ilinyakua dhahabu 6, fedha 2 na shaba 2, wakati wenzao wa chini ya umri wa miaka 18 wakizoa medali 19, dhahabu 6, fedha 7 na sahaba 6.
Wanariadha hao watasafiri kesho usiku kuelekea Nigeria.