Wanariadha 150 wamealikwa kushiriki majaribio ya kitaifa ya Julai 22 kuteua kikosi cha Kenya kwa mashindano ya Riadha Duniani Septemba mwaka huu.
Majaribio hayo yataandaliwa katika uwanja wa Ulinzi Complex.
Wanariadha walioalikwa ni wale waliotimiza masharti yaliyowekwa, ikiwemo vipimo vitatu vya ulaji muku na kutimiza muda wa kufuzu.
Bingwa mtetezi katika mita 1500 na mita 5000 Faith Kipyegon amepewa tiketi ya moja kwa moja sawia na Mary Moraa katika mita 800.