Wanamgambo watano wa Al Shabaab wauawa Lamu na wanajeshi wa KDF

Washukiwa hao wameuawa kwenye uvamizi wa KDF uliotekelezwa katika eneo la Lacta Mangai, katika msitu wa Boni kaunti ya Lamu.

Dismas Otuke
0 Min Read

Wanajeshi  wa Kenya wamewaua washukiwa watano wa wanamgambo wa Al Shabaab katika kaunti ya Lamu.

Washukiwa hao wameuawa kwenye uvamizi wa KDF uliotekelezwa katika eneo la Lacta Mangai, katika msitu wa Boni kaunti ya Lamu.

Yamkini pia wanamgambo wengine wametoweka wakiwa na majeraha.

Wanajeshi hao pia walipata silaha kadhaa zikiwemo bunduki za AK-47, roketi za kurusha gruneti, viwambo vya sola, hema na vifaa vya kutengeneza vilipuzi.

Share This Article