Wanajeshi watatu wafariki kwenye shambulizi la kilipuzi Lamu

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamume awaua wanawe wawili kabla ya kujitoa uhai Mai Mahiu.

Maafisa watatu wa Vikosi Vya Ulinzi Nchini (KDF), wameaga dunia baada ya kilipuzi kulipuka katika eneo la Sankuri, kaunti ya Lamu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka KDF, kifaa hicho kililipuka kwenye barabara ya Sankuri-Kiunga wanajeshi hao walipokuwa wakishika doria.

Taarifa inaelezea kuwa wanajeshi waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali za kijeshi zilizo eneo hilo ili kupokea matibabu ya kitaalam.

Vikosi vya Ulinzi vimesema, kundi la asasi mbalimbali limetumwa kuwatafuta waliotekeleza shambulizi hilo na kuimarisha usalama katika eneo hilo.

“Vikosi vya Ulinzi vinatambua ujasiri uliodhihirishwa na maafisa wetu, na kupongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na kundi la maafisa wa asasi mbalimbali katika eneo hilo,” ilisema taarifa ya KDF.

TAGGED:
Share This Article