Maafisa wa serikali ya Nigeria, wamefanikiwa kuwaokoa wanafunzi 100 waliokuwa wametekwa kutoka shule moja ya kikatoliki mwezi uliopita.
Hata hivyo wanafunzi wengine 165, bado hawajulikani waliko.
Kulingana na vyanzo vya habari, wanafunzi hao watakabidhiwa kwa maafisa wa serikali leo Jumatatu, kabla ya kujiunga na familia zao.
Wakati huo huo, mshauri wa Usalama wa Taifa, Nuhu Ribadu alifanya ziara Papiri wiki iliyopita na kukutana na ujumbe ulioongozwa na mmiliki wa shule hiyo, Askofu Yohanna, aliwahakikishia kwamba watoto hao wataokolewa hivi karibuni na kuungana tena na familia zao.
Aidha, wazazi wa watoto hao wamesema wanasubiri kwa hamu kubwa taarifa kuhusu watoto wao.