Wanabodaboda katika kaunti ya Trans Nzoia wameanzisha vuguvugu lao la kuwaunganisha ili kuimarisha mtaji wao kupitia kuwekeza kwa ushirika huku wakiwaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia vibaya.
Wanabodaboda hao wanasema imekuwa vigumu wao kupata mkopo kununua pikipiki au kuimarisha biashara yao ya bodaboda kwa sasa wakisema umoja wao utawasaidia kufaidika kupitia ushirika.
Wakizungumza mjini Kitale baada ya kupokea hundi ya shilingi nusu millioni kutoka hazina ya eneo bunge la Kiminini, viongozi wa wanabodaboda hao wameonya wenzao dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa wakati huu ambapo joto la siasa ya mwaka wa 2027 limeanza kupanda, badala yake kuungana kufanya biashara ya kuwakwamua kutoka kwa umaskini.