Wallace Karia achaguliwa tena Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF

Karia ameibuka mshindi kwenye uchaguzi ambao umeandaliwa leo Jumamosi, Agosti 16, mjini Tanga.

Dismas Otuke
0 Min Read

Wallace Karia amechaguliwa tena kuongoza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Karia ameibuka mshindi kwenye uchaguzi ambao umeandaliwa leo Jumamosi, Agosti 16, mjini Tanga.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Kiomoni Kibamba, amemtangaza Karia kuwa mshindi.

Awali, Karia alikuwa Rais wa CECAFA na anaanza kuhudumu kwa muhula wa tatu kuongoza TFF, baada ya kuwa afisini kwa miaka minane.

Share This Article