Utekaji nyara wa Koimburi: Washukiwa watatu wafikishwa mahakamani

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa katika sakata ya kutekwa nyara kwa mbunge wa Juja George Kuimburi wafikishwa mahakamani.

Washukiwa waliokamatwa kuhusiana na sakata ya utekaji nyara bandia wa mbunge wa Juja George Koimburi, wamefikishwa mahakamani leo Ijumaa.

Maafisa wa polisi ambao wanaendelea na uchunguzi, wamewasilisha ombi mahakamani kuendelea kuwazuilia washukiwa hao kwa siku 15 zaidi, huku wakiendelea na uchunguzi wa kubainisha chanzo cha utekaji nyara huo.

Mwakilishi wadi wa Kanyenyaini kaunti ya Murang’a Grace Nduta, ni miongoni mwa wanaozuiliwa na polisi kuhusiana na kisa hicho.

Nduta alitiwa nguvuni siku moja baada ya maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, kusema wamepata gari la kibinafsi ambalo lilitumiwa katika utekaji nyara huo.

“Tungependa kuthibitisha kuwa Grace Nduta Wairimu, anayewakilisha Wadi ya Kanyenyaini, Kaunti ya Murang’a, alikamatwa Mei 29,2025 kama sehemu ya uchunguzi kuhusiana na sakata ya kutekwa nyara kwa mbunge George Koimburi”,ilisema taarifa ya DCI.

Koimburi angali amelazwa katika hospitali ya Karen, Jijini Nairobi.

Share This Article