Waliojihusisha na biashara ya pombe haramu awali wakabidhiwa ng’ombe wa maziwa Nandi

Marion Bosire
1 Min Read

Kina mama zaidi ya 300 wamesherehekewa na kupatiwa ng’ombe wa maziwa Katika kijiji cha Kapng’ombe, eneo bunge la Mosop, kaunti ya Nandi.

Awali kina mama hao walijihusisha na utengenezaji na uuzaji wa pombe isiyokubalika Katika jamii.

Priska Magut ni mmoja wa kina mama hao anayesimulia jinsi maisha yake yamebadilika baada ya kujihusisha na pombe hiyo haramu kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya kurudishwa shuleni kusoma akiwa na umri wa miaka 31 hadi akawa mwalimu wa sekondari.

Kina mama hao sasa wanaomba mashirika mbali mbali yajitokeze na yashirikiane na serikali zote mbili ya kitaifa na ya kaunti, ili kuhamasisha walioathirika na wasiojiweza katika maeneo tofauti kuhusu athari za pombe hali ambayo imechangia umaskini kushamiri Katika jamii.

Mary Tarkok Rono ambaye ni msimamizi wa Shirika la Hope for Change anasema ipo haja ya waathiriwa hao kupatiwa usaidizi wa kipekee na mafunzo ya kutosha ili waweze kujikimu kimaisha.

Kwa sasa makundi ya kina mama zaidi ya 20 yamenufaika na mpango huo wa hivi punde huku Ngombe zaidi ya 5000 wakikabidhiwa wasiojiweza katika eneo la Bonde la ufa kwa muda wa miaka 10 iliyopita na Shirika hilo linalolenga kufikia Kaunti zote nchini.

Share This Article