Walimu kula unono kuanzia mwisho wa Julai

TSC itatakeleza nyongeza mpya ya mishahara ya walimu kwa kipindi cha miaka minne kwa gharama ya shilingi bilioni 33.8.

Dismas Otuke
1 Min Read

Walimu kote nchini wanatarajiwa kupata nyongeza ya mshahara kati ya asilimia 5 na 29.6, kuanzia mwisho wa mwezi huu wa Julai.

Hii ni kufuatia kusainiwa kwa makubaliano mapya ya nyongeza mpya ya mishahara ya walimu baina ya tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC, na vyama vitatu vya walimu: KUPPET, KNUT na KUSNET.

TSC itatakeleza nyongeza mpya ya mishahara ya walimu kwa kipindi cha miaka minne kwa gharama ya shilingi bilioni 33.8.

Chini ya makubaliano hayo, walimu watakuwa wakipata nyongeza ya mishahara kila mwaka katika muda wa miaka minne.

Share This Article