Wakurugenzi wa halmashauri mbili za barabara hapa nchini, wamejiuzulu kutoka kwa nyadhifa zao mara moja.<
Mhandisi Kungu Ndungu, amejiuzulu wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Barabara Kuu Nchini (KeNHA), kulingana na taarifa kutoka bodi ya wakurugenzi.
Wadhifa wa mhandisi Kungu sasa umechukuliwa na mhandisi Luka Kimeli, ambaye atakaimu wadhifa huo mara moja.
Kwa upande mwingine Mhandisi Philemon Kandie amejiuzulu wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Barabara za Mashinani (KeRRA), kuanzia Julai 11, 2025.
Tangazo hilo lilitolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya KeRRA’s, ambayo pia ilimtaja Mhandisi Jackson K. Magondu, Mkurugenzi wa Mipango na Mazingira kukaimu wadhifa huo baada ya mashauriano na waziri wa Barabara na Uchukuzi.
“Halmashauri hii ingependa kufahamisha umma kujiuzulu kwa Mhandisi Philemon Kandie, kama Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Barabara za mashinani kuanzia Julai 11, 2025,”ilisema taarifa hiyo.
Bodi hiyo ya Wakurugenzi ilimpongeza Kandie kutokana na mchango wake na huduma alizotoa kwenye bodi halashauri hiyo.