Wakili bandia akamatwa Machakos

Tom Mathinji
1 Min Read
Wakili bandia akamatwa Machakos.

Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) kwa ushirikiano na maafisa wa polisi, wamemtia nguvuni wakili bandia mjini Machakos.

Mshukiwa huyo ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya mawakili ya C.M Maweu kwa muda wa miaka mitatu bila stakabadhi zozote kuonyesha amehitimu au kusajiliwa, amekuwa akiwahadaa wananchi kwa kutoa huduma za uwakili.

Kulingana na mwanachama wa baraza la LSK Wavinya Nicholas aliyeongoza operesheni hiyo, Chama cha LSK kilikuwa kinatekeleza ukaguzi wa kampuni zote zinazotoa huduma za mawakili katika kauntinya Machako, baada ya kupokea habari kutoka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa mawakili bandia.

“Tumepokea habari muhimu kutoka kwa umma na kwa wanachama wa LSK akuhusu ongezeko la mawakili bandia Machakos na tumemkamata mshukiwa mmoja,” alisema Wavinya.

Aliwaonya wananchi kuwa makini dhidi ya kutapeliwa na mawakili bandia, akiwataka kutafuta huduma kwa mawakili waliosajiliwa na chama cha LSK.

TAGGED:
Share This Article