Wakenya watakiwa kuzingatia maadili wanapowachagua viongozi

Martin Mwanje
1 Min Read

Huku mdahalo wa kukithiri kwa ufisadi bungeni ukiendelea kushika kasi, Wakenya na viongozi wa makanisa wametakiwa kuwachunguza viongozi kabla ya kuwachagua.

Kwa mujibu wa msomi wa maswala ya uongozi Prof. Joseph Nzioka, aliyezungumza katika eneo la Kivaa, Yatta, katika kaunti ya Machakos, ipo haja kubwa ya Wakenya kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili wanapowachagua viongozi ili kuokoa taifa la Kenya dhidi ya uongozi mbaya na kuwezssha uwepo wa maendeleo katka kila pembe ya nchi.

Aidha, Prof. Nzioka amewataka viongozi wa kidini kuwa na msimamo mkali dhidi ya wanasiasa wafisadi nchini ili kupigania haki ya Wakenya ambao wengi wanaendelea kuteseka kwa kukosa pato la kila siku.

Amewalaumu viongozi wa eneo la Yatta kwa kukosa kuleta maendeleo ya miundombinu ya kawaida katika eneo hilo lenye hifadhi ya maji ya bwawa la Masinga.

Kulingana naye, eneo hilo limesalia nyuma kimaendeleo kwa muda mrefu kutokana na uongozi mbaya.

Share This Article